Saturday, February 25, 2017

TAMKO LA CHAMA HA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA ( TAMRA )







TAMKO LA CHAMA HA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA ( TAMRA )
25.02.2017.
Tamko  la chama  cha  kutetea  haki za wanaume Tanzania kuhusiana na tukio la mauaji ya yaliyofanywa  na  Mohamed Mohamed mkazi wa  boko Jijini Dar es salaam tukio ambalo limeteka hisia za wengi  kuwa mwanaume huyo ametenda kosa bila kuangalia pande zote ili kujua chanzo cha tatizo la wanandoa hao
Chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania TAMRA kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mauaji yaliyotokea huko boko Dar  es salaam  kutokana na hatua zilizochukuliwa na mmoja wa wanaume aitwaye Mohamed Mohamed (46) mfanyabiashara mkazi wa boko  jijini dar es salaam kwa kumuua mkewe sophia(36) na kisha yeye mwenyewe kujiua na kuacha ujumbe kurasa 80 ujumbe ambao  kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi ndiyo umebeba sababu mauaji hayo
Kimsingi,jamii imekwenda mbali katika tukio hili kwa kuwachukulia wanaume kuwa ni wabaya,ni katili, sawa lakini chama hiki kinaomba jamii itambue uwepo wa migogoro mikubwa inayofukuta ndani ya ndoa zetu huku chanzo kikubwa kikiwa ni baadhi ya akina mama,nasema hivyo kutokana na ushahidi kwamba,tafiti zilizofanyika hapo nyuma zilionyesha kuwa katika mikoa minne ikiwemo lindi mtwara dar es salaam na zanzibar ilionyesha kuwa wanawake walikuwa wakiongoza kwa kupiga wanaume ikiwamo kuwanyima unyumba huku wanaume wakikosa pa kusemea kutokana na kutokuwepo kwa chombo hiki mpaka pale chama hiki kilipoanzishwa .
Matatizo mengine ukiachilia kupigwa wanaume wamekuwa wakipambana na vituko vingi ikiwemo ukatili wa kijinsia kwa kutengwa na familia wakiwemo watoto kuambatana na misimamo ya mama huku baba akibaki mkiwa na baadaye kupelekea vifo vingi kwa akina baba.
Tafiti zinaonyesha kuwa wanaoathirika zaidi ni wanaume hasa waliostaafu kazi serikalini taasisi na mashirika kwamba wanapokuwa wamekoma kupata fedha kwa ajiri ya kutunza familia hutengwa na baada ya muda huugua magonjwa makubwa ikiwemo kupooza,sukari,nk.
Yote haya yanatokana na mwanaume kushindwa kuthaminiwa utu wake na kudharauliwa na familia na hapo ndipo hujikuta katika lindi la mawazo na kupelekea kupoteza maisha.
katibu mkuu wa chama cha kutetea haki za wanaume Antony Sollo amejaribu kufuatilia suala hili kuona jamii imelipokeaje tukio hili ambapo watu mbali mbali wameweza kuelezea hisia zao
akizungumza na katibu mkuu wa tamra seif hemed mkazi wa uhuru jijini mwanza ametoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo na kusema kwamba tukio hili limesababishwa na mwanamke kutokana na majibu aliyokuwa akimjibu mwanandoa mwenzake hususani pale alipotamka kwamba watoto waliozaa si wake,matumizi mabaya ya fedha za mmewe jambo ambalo linaumiza moyo
“hata kama nngekuwa mimi nisingeweza kuvumilia kwa kuwa mke nimeshiriki kumtafuita kumlipia mahari,kumtunza kwa kumpatia mahitaji mbalimbali ikiwemo kulea ujauzito na kuwalea watoto nikijua ni mali yangu halafu leo mtu anaibuka na kusema kuwa watoto hawa si wangu inauma sana alisema seif”.
kufuatia hali hii tamra haina ugomvi na wanawake ila inawataka wanandoa kuheshimu ndoa kwani ni agizo la mungu kwamba enendeni mkazaliane muijaze dunia ambapo baada ya agizo hilo muungu aliagiza mambo mawili ikiwemo wajibu wa kila mwanandoa.
iwapo wanandoa watamheshimu mungu na kutekeleza wajibu wao kila mmoja ndoa hizo zitadumu na amani ndani ya ndoa hizo itakuwa ni ya milele.
Haya ni Maagizo ya mungu kwa wanandoa.
kwa wanawake : WAEFESO 5 : 22 neno la Mungu linasema enyi wake watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu , kwa maana Mume ni kichwa cha Mkewe,kama kristo naye ni kichwa cha kanisa naye ni mwokozi wa mwili lakini kama vile kanisa limtiivyo kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
Kwa Wanaume: Waefeso 5: 25 Enyi waume wapendeni wake zenu kama kristo naye alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajiri yake,ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayobali liwe takatifu lisilo na mawaa vivyo hivyo imewapasa waume zao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe,hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote bali huulisha na kuutunza kama kristo naye alivyolitendea kanisa.
Hivyo nachukua nafasi hii kuiomba jamii mambo yafuatayo
1.      Kuheshimu neno la Mungu ili kuweza kudumisha ndoa zetu.
2.      Kuwa wavumilivu katika shida na raha kama viapo tulivyoapa mbele za Mungu
3.      Tuweze kujifunza masomo ya ndoa ili kuingia katika ndoa tukiwa na ujuzi juu ya wajibu wetu baada ya kuingia katika Tasnia hii muhimu ya ndoa.
4.      Tumtegemee Mungu katika mambo yote na tukio hili liwe fundisho kwetu tujipeleleze ni wapi tuna Mgogoro usioisha katika ndoa zetu ili kuepuka Mauaji ya aina hii.
IMEANDALIWA NA:
Antony Johnson Sollo
KATIBU MKUU TAMRA TANZANIA
1.      0767 203 556  BERENS CHINA                        Mwenyekiti  TAMRA
2.      0762  117 117  ANTONY JOHNSON SOLLO  Katibu Mkuu TAMRA

Wednesday, November 2, 2016

CAG abainisha Madudu Misungwi


Na Antony Sollo Misungwi

MZIMU wa Hati yenye Mashaka umezidi kuiandama Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,hii ni baada ya ripoti iliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali CAG kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2014/15.

Kufuatia ripoti ya CAG,Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imepata Hati yenye Mashaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Halmashauri hiyo kudaiwa madeni na watu mbalimbali yanayofikia shilingi 472,018,814.

Hoja zingine za ukaguzi zilizotolewa katika ripoti ya CAG ni kuwepo kwa malipo ya mishahara yaliyofanywa kwa watumishi waliokoma utumishi ( hewa )walioisabishia Serikali kiasi cha shilingi 12,483,000,ununuzi wa mafuta hewa kiasi cha shilingi 43,399,972,ununuzi wa mafuta kwa ajiri ya magari binafsi kwa kutumia mwamvuli wa Serikali shilingi 7,815.450.

Ripoti hiyo pia imeonyesha utekelezaji wa miradi ya maji ya bomba ambayo imeigharimu Halmashauri hiyo mamilioni ya shilingi kama ifuatavyo,mradi wa maji ya bomba Ngaya/Matale shilingi 305,058,000,mradi wa maji ya bomba kijiji cha Bujingwa shilingi 293,590,000.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji ya bomba tayari Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda amefanya ziara ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali na kubaini madudu hayo na kuagiza taasisi mbalimbali likiwemo Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru kufanya Uchunguzi hatimaye wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufikishwa Mahakamani.

Kufuatia madudu hayo, Diwani wa Kata ya Mabuki Nicodemus Ihano ( CCM ) alisimama na kuhoji kuhusu mapungufu ya taarifa mbalimbali zilizotolewa katika baraza lililokaa 18 August mwaka huu lakini alitolewa nje ya ukumbi wa Mkutano na Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya ya Misungwi Antony Bahebe kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Kiongozi mmoja kutoka ndani ya CCM aliwaambia Mwandishi wa Habari hizi kuwa kuna udanganyifu mkubwa uliofanyika wakati wa upatikanaji wa tenda na utekelezaji wa  ujenzi wa miradi ya maji huku Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga akihusishwa kuwa na maslahi katika miradi hiyo.

“kuna tatizo kubwa juu ya upatikanaji wa Mkandarasi wa Mradi wa maji kwani Mbunge alileta Kampuni moja kutoka Dar es salaam ambayo mmiliki wake wana urafiki,si hivyo tu hata Mwenyekiti wetu wa Halmashauri ya Wilaya Antony Bahebe ndiye msimamizi wa mradi ambapo tunashangazwa na vitendo vya viongozi hawa kujiingiza katika kusimamia kampuni kwa maslahi binafsi”alisema kiongozi huyo ambaye hata hivyo hakutaka kuandikwa jina lake kwenye gazeti.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi  Eliud Mwaiteleke alipotafutwa kuzungumzia ripoti hiyo alisema kuwa yuko msibani hivyo yafanyike mawasiliano kwa ujumbe mfupi wa maandishi ambapo hata hivyo alijibu kwa hasira kuwa hana majibu juu ya ripoti hiyo

Kwa upande wake Mbunge wa JImbo la Misungwi Charles Kitwanga alipotafutwa kwa njia ya simu simu yake iliita bila majibu hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu chochote na baadaye simu yake ilizimwa.









Tuesday, October 25, 2016

Ajichinja kwa wivu wa Mapenzi






Ajichinja kwa wivu wa Mapenzi
Na Antony Sollo Mpwapwa.

Mtu mmoja amenusurika kifo katika stendi ya mabasi Wilayani Mpwapwa baada ya kujichinja kwa kutumia kitu chenye ncha kali kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea Oktoba 25 majira ya saa 7: 53 mchana katika stendi ya mabasi Wilayani Mpwapwa, mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alichukua uamzi huo baada ya kukataliwa na mwanamke aliyedaiwa kuwa alikuwa ni mpenzi wake.

Chanzo cha taarifa kutoka Wilayani Mpwapwa zimeeleza kuwa kijana huyo ni mgeni katika maeneo hayo na kwamba alikuja kumfuatilia mpenzi wake akitokea Mkoani Iringa ambapo baada ya kufika katika maeneo hayo,alikuta mpenzi wake akiwa na mwanamme mwingine jambo lililosababisha kuchukua uamzi wa kujitoa roho

Hata hivyo juhudi za kujitoa uhai kwa kijana huyo ziligonga mwamba baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kufika katika eneo la tukio kumchukua na kumkimbiza  hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kwa matibabu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi kuzungumzia tukio hilo simu yake iliita bila majibu na juhudi za kumtafuta zinaendelea ili kuweza kuthibitisha taarifa  hizo

Sunday, October 23, 2016

TANGAZO KWA WANAUME WOTE TANZANIA


Wadau wa Chanma cha kutetea Haki za wanaume Tanzania napenda kuwataarifu kuwa tunarudi kuwaletea matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa Haki za Wanaume Nchini Tanzania na Duniani kote.
Karibuni saaana!