Mh
Waziri,
Naomba
kuwasilisha Malalamiko yangu kwako kuhusu vitendo nilivyofanyiwa na
kampuni
ya Tujijenge Microfinance iliyoko katika mtaa wa New
Bagamoyo Rd. Plot 17, Block 45A yenye Makao yake Makuu jijini Dar es salaam Dar Es salaam
Mimi ni mwananchi mkazi wa jiji la Dar es
salaam, niliomba Mkopo wa Shilingi milioni arobaini (40,000,000/) kwa ajili ya
kuimarisha biashara yangu tangu 25 March mwaka huu na kutimiza masharti ikiwemo
kufanyiwa tathmini ya biashara yangu hivyo
kukubaliwa kupatiwa fedha nilizoomba lakini hadi sasa niko njiapanda sijui la
kufanya japokuwa kwa mujibu wa mashharti ya Kampuni hiyo nilitakiwa niwe nimepatiwa mkopo huo ndani ya
siku saba baada ya kukamilisha masharti ya mkopo huo.
Mh Waziri
nimesikitishwa na watendaji wa Shirika hilo baada ya kuniingiza katika mgogoro
mkubwa kutokana na kuchukua mkopo katika taasisi ndogo za fedha baada ya kuhakikishiwa kuwa nimefuzu
kupatiwa mkopo huo ndani ya siku saba lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea.
Nilikuwa na
mpango wa kukuza biashara yangu kwa kununua basi kwa ajili ya kusafirisha
wanafunzi ,nimesumbuliwa sana,nimetumia zaidi ya shilingi milioni mbili kwa
ajili ya mawasiliano usafiri paomja na muda na kuingia madeni yaliyopelekea
kuchukuliwa vitu vyangu nilivyoweka kama dhamana .kutokana na ahadi niliyokuwa
nimetoa kwa wateja wangu kwamba ningekamilisha suala hilo kwa muda lakini hadi
sasa sijui kinachoendelea.
Kufuatia
hali hii nimeingia gharama kubwa
yakiwemo madeni kutokana na ahadi za watendaji wa Kampuni hii
zinazofikia mil 2 pamoja na kuchukuliwa kwa mali zangu zenye thamani zaidi ya
shilingi milioni nane ambapo jumla ya madai yote ni shilingi milioni kumi(
10,000,000 ) na ninaomba uingilie kati mgogoro huu kufuatia baadhi ya taasisisi za fedha kuendesha shughuli zao bila
kuzingatia Sheria za Nchi.
Nimejitahidi
kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu bila mafanikio sasa naomba msaada maana mpaka
sasa nimeingia katika matatizo makubwa ikiwemo kuyumba kwa uchumi na mahitaji
ya familia maana nimetumia fedha nyingi katika ufuatiliaji ikiwemo kuweka
mafuta kwenye magari ya maafisa wa Shirika hilo kwa nyakati tofauti hasa baada
ya kuhakikishiwa kuwa nimefuzu kupata mkopo lakini hadi sasa nimetelekezwa.
Kwa
barua hii naiomba Serikali iingilie kati suala hili ili haki iweze kutendeka.
BARAKA BEATUS MASHAURI
S L P
DAR ES
SALAAM