KITWANGA
ACHARUKA SAKATA LA KIWANDA CHA SAYONA KUNYANYASA WAFANYAKAZI.
Na
Antony Sollo -Mwanza.
15 April
2013
Mbunge wajimbo la Misungwi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
Charles Kitwanga ‘Mawe Matatu”amesema kuwa iwapo manyanyaso wanayopata wafanyakazi
na wananchi walioko katika kiwanda cha Sayona kilichopo eneo la Nyang’homango
kata ya Usagara Jijini Mwanza hayatakomeshwa na vyombo vinavyohusika ataiacha Ofisi
yake kwenda kushughulika na suala hilo mpaka kieleweke.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza na Mwanaharakati
wa Haki za Binadamu aliyetembelea Kiwanda cha Sayona na kujionea jinsi wananchi
pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho wanavyonyanyaswa na mwekezaji wakiwanda hicho.
Kitwanga alisema kuwa amesikitishwa na taarifa iliyotolewa kwake na mwanaharakati
huyo ambapo taarifa hiyo ikionyesha mapungufu makubwa yaliyopo katika kiwanda
cha Sayona hususani katika kulinda maslahi ya wafanyakazi ikiwemo ukiukwaji wa Haki
za binadamu na ukiukwaji wa Sheriaya Fidia kwa Wafanyakazi
(Workmens’ Compensation Ordinance),
Cap.263 ya 1948.
Sheria
hii ilitungwa ilikutoa fidia kwa wafanyakazi wanaopata ajali au maradhi yanayotokana
nakazi. Sheria hii pia inakwenda sambamba na sheria ya kutaarifua Ajari na maradhi
yatokanayo na kazi ambayo iliitwa
“Accidents and Occupational Diseases” (Notification) Ordinance, Cap 330.
Mwaka1953
marekebisho yalifanyika katika sheria hiyo (Sura 263) kwa
Kutungasheria
nyingine Na. 25 ya1953 ambayo ilikuwa na lengo la
Kumlazimisha
mwajiri kutoa taarifa kwa Afisa Kazi wa eneo husika
Pale mfanyakazi
anapoumia au kupata ugonjwa unaotokanana
kazi.
Taarifa hiyo pia ilionyesha
mambo mengi ikiwemo kutotolewa kwa taarifa kwa uwazi kuhusu matukio yanayotokea
kiwandani hapo ikiwemo milipuko inayotokea na jinsi wahanga wa milipuko hiyo wanavyohudumiwa
na haki zao kuhusu kuumia pamoja na vifo vinavyotokea ikiwamo na fidia wanazopaswa
kulipwa wahanga na familia za wafanyakazi waliokufa wakiwa kazini.
Imegundulika kuwa Wafanyakazi wa kiwanda cha Sayona kuwa hufukuzwa bila kufuatwa kwa kanuni na taratibu
kwa mujibu wa Sheria za kazi ambapo Sheriaya Ajira (Employment Ordinance),
Cap.366 ya 1957 jambo ambalo
linavunja uwepo wa Sheria Na.82 ya mwaka 1962,iliyotungwa
ili kuongeza marupurupu mbalimbaliYa mfanyakazi
kama vile, mafao ya kuachishwa kazi, likizo na huku
Sheria
ya kiinua mgongo “Severance Allowance Act” Na. 57 ya mwaka
1962,ikitoa haki na utaratibu wamalipo ya kujikimu baada
ya kuachishwakazi.
Wafanyakazi
hao pia wamelalamikia uvunjwajiwa Sheria Na.62 ya mwaka1964, Sheria
ya Usalama Kazini(Security of Employment Act) kwa kufanyishwa kazi masaa
mengi bila kupumzika jambo ambalo inasemekana kuwandiyo chanzo cha Ajari Sheria hii ilianzishwa ilikupunguza uwezo
wa waajiri kuajiri na kufukuza wafanyakazi na kuainisha aina za makosa na adhabu
zake.
Rekebisho
la Sheria Namba 17 la mwaka1983.lililenga kubadilisha
Viwango
vya juu vya malipo kwa ulemavu wa kudumu na magonjwa
Yatokanayo
na kazi kutoka shilingi 36,000/= hadi shilingi 108,000/= na
Kwa vifo
kutoka shilingi 29,000/= hadi shilingi 83,000/=
Wakala
wa Afyana Usalama Mahali pa kazi (OSHA) ulianzishwa
kwa lengo la kusimamia masuala yote ya afya na usalama sehemu za kazi ili kupunguza
ajari na magonjwa yatokanayo na kazi na hatimaye kuongeza tija.
Aidha
kwa kupitia wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi (OSHA) Wizara imefanikiwa kufanya kaguzi kama inavyoonyeshwa katika
Jedwali
hapa chini
MWAKA
|
KUPIMA AFYA
|
KAGUZI ZA
KAWAIDA
|
KAGUZI
MAALUM
|
2001-2005
|
23,864
|
26,000
|
9,612
|
2006-2010
|
44,463
|
22,234
|
50,979
|
JUMLA
|
68,327
|
31,846
|
76,979
|
Kutokana
na kaguzi hizo, wakala umeweza kubaini baadhi ya waajiri ambao
Hawatoi
taarifa za ajari zinapotokea na ambao hawasajili sehemu za kazi na
Kuchukuliwa
hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na wengine
Kupelekwa
kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa hatua zaidi.
Akizungumza
na Tanzania daima Afisa mmoja wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi Mkoani
Mwanza ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama ameliambia
Tanzania daima kuwa ni kweli upo uzembe uliobainika katika Kiwanda cha Sayona katika
kipindi cha mwaka 2012 ambapo Kiwanda
cha Sayona kimetozwa faini mara mbili mfurulizo kutokana na uzembe na huduma duni
katika masuala ya Usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi
wake.
HAWA NDIYO MOJA WA MAJERUHI WA KIWANDA CHA SAYONA JIJINI MWANZA WAKIHANGAIKA NA VIDONDA
BAADA YA KULIPUKIWA NA JIKO LA KUYEYUSHIA VYUMA KATIKA KIWANDA CHA HICHO.
Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona LUCAS LUBINZA akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO
Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona Lucas Nkalango akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO
Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona LUCAS LUBINZA akiwa ameumia vibaya sehemu ya nyuma baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO
Kwa upande wa nyuma anavyoonekana Lubinza akiwa ameungua vibaya