TAMRA itakuwa na malengo kama ifuatavyo:-
(1) Kupigania Haki za mwanaume katika masuala mbalimbali ikiwamemo kulinda na kuidumkisha ndoa.(2) Kulinda Haki ya mwanaume ngazi ya familia ,kitaifa na kimataifa.
(3) Kuelimisha waathirika wa unyanyasaji
(4) Kutoa msaada wa kisheria.
(5) Kutoa elimu ya Afya na malezi ya mototo wa kiume ili akue katika maadili yanayozingatia haki sawa kwa wote bila.
(6) Kutoa elimu juu ya magonjwa yasiyokuwa na tiba ikiwamo Ukimwi (HIV/AIDS).
(7) Kutoa elimu na mafunzo kwa wanamme ili kuwafundisha ujasiria mali kuondoa utegemezi.
(8) Kufanya upatanishi na usuluhishi kwa wanandoa.
(9) Kutoa elimu kwa wanaume kukubali mabadiliko ya mwili kufuatana na umri kuwa mkubwa kati ya mwanamme au mwanamke.
(10) Kutoa mawakili wa chama kwenda mahakamani kutetea wanaume walio na kesi kutokana na na vitendo vya unyanyasaji ili kuhakikisha haki inatendeka kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za nchi bila kuathiri haki za binadamu.
(11) Kudumisha amani ya nchi.
(12) Kulinda Haki za kila raia bila kujali itikadi za dini, rangi, kabila jinsia na taifa.
(13) Kusimamia na kulinda mazingira, elimu ya uraia.
(14) Kushirikiana na serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa katika siku ya mwanamme Duniani ikiwemo kuandaa sherehe hiyo kitaifa na kimataifa.
(15) Kutoa misaada kwa makundi ya wasiojiweza yatima, wazee,wagonjwa ,wakimbizi majeruhi wa ajari, majanga kama njaa,mafuriko, shule au kujenga majengo ya kutoa huduma za afya na elimu kulinda na kutunza mazingira kuangalia chaguzi ndani na nje ya Tanzania.