Monday, April 15, 2013

KITWANGA ACHARUKA SAKATA LA KIWANDA CHA SAYONA KUNYANYASA WAFANYAKAZI



KITWANGA ACHARUKA SAKATA LA KIWANDA CHA SAYONA KUNYANYASA WAFANYAKAZI.
Na Antony Sollo  -Mwanza.
15 April 2013
Mbunge wajimbo la Misungwi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Charles Kitwanga ‘Mawe Matatu”amesema kuwa iwapo manyanyaso wanayopata wafanyakazi na wananchi walioko katika kiwanda cha Sayona kilichopo eneo la Nyang’homango kata ya Usagara Jijini Mwanza hayatakomeshwa na vyombo vinavyohusika ataiacha Ofisi yake kwenda kushughulika na suala hilo mpaka kieleweke.
 
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu aliyetembelea Kiwanda cha Sayona na kujionea jinsi wananchi pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho wanavyonyanyaswa na mwekezaji wakiwanda hicho.
Kitwanga alisema kuwa amesikitishwa  na taarifa iliyotolewa kwake na mwanaharakati huyo ambapo taarifa hiyo ikionyesha mapungufu makubwa yaliyopo katika kiwanda cha Sayona hususani katika kulinda maslahi ya wafanyakazi ikiwemo ukiukwaji wa Haki za binadamu na ukiukwaji wa Sheriaya Fidia kwa Wafanyakazi (Workmens’ Compensation Ordinance), Cap.263 ya 1948.
Sheria hii ilitungwa ilikutoa fidia kwa wafanyakazi wanaopata ajali au maradhi yanayotokana nakazi. Sheria hii pia inakwenda sambamba na sheria ya kutaarifua Ajari na maradhi yatokanayo na kazi ambayo iliitwa “Accidents and Occupational Diseases” (Notification) Ordinance, Cap 330.

Mwaka1953 marekebisho yalifanyika katika sheria hiyo (Sura 263) kwa
Kutungasheria nyingine Na. 25 ya1953 ambayo ilikuwa na lengo la
Kumlazimisha mwajiri kutoa taarifa kwa Afisa Kazi wa eneo husika
Pale mfanyakazi anapoumia au kupata ugonjwa unaotokanana
kazi.
Taarifa hiyo pia ilionyesha mambo mengi ikiwemo kutotolewa kwa taarifa kwa uwazi kuhusu matukio yanayotokea kiwandani hapo ikiwemo milipuko inayotokea na jinsi wahanga wa milipuko hiyo wanavyohudumiwa na haki zao kuhusu kuumia pamoja na vifo vinavyotokea ikiwamo na fidia wanazopaswa kulipwa wahanga na familia za wafanyakazi waliokufa wakiwa kazini.

Imegundulika kuwa Wafanyakazi wa kiwanda cha Sayona  kuwa hufukuzwa bila kufuatwa kwa kanuni na taratibu kwa mujibu wa Sheria za kazi ambapo Sheriaya Ajira (Employment Ordinance), Cap.366 ya 1957  jambo ambalo linavunja uwepo wa Sheria Na.82 ya mwaka 1962,iliyotungwa ili kuongeza marupurupu mbalimbaliYa mfanyakazi kama vile, mafao ya kuachishwa kazi, likizo na huku
Sheria ya kiinua mgongo “Severance Allowance Act” Na. 57 ya mwaka
1962,ikitoa haki na utaratibu wamalipo ya kujikimu baada ya kuachishwakazi.
Wafanyakazi hao pia wamelalamikia uvunjwajiwa Sheria Na.62 ya mwaka1964, Sheria ya Usalama Kazini(Security of Employment Act) kwa kufanyishwa kazi masaa mengi bila kupumzika jambo ambalo inasemekana kuwandiyo chanzo cha  Ajari Sheria hii ilianzishwa ilikupunguza uwezo wa waajiri kuajiri na kufukuza wafanyakazi na kuainisha aina za makosa na adhabu zake.

Rekebisho la Sheria Namba 17 la mwaka1983.lililenga kubadilisha
Viwango vya juu vya malipo kwa ulemavu wa kudumu na magonjwa
Yatokanayo na kazi kutoka shilingi 36,000/= hadi shilingi 108,000/= na
Kwa vifo kutoka shilingi 29,000/= hadi shilingi 83,000/=

Wakala wa Afyana Usalama Mahali pa kazi (OSHA) ulianzishwa kwa lengo la kusimamia masuala yote ya afya na usalama sehemu za kazi ili kupunguza ajari na magonjwa yatokanayo na kazi na hatimaye kuongeza tija.

Aidha kwa kupitia wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi (OSHA) Wizara imefanikiwa kufanya kaguzi kama inavyoonyeshwa katika
Jedwali hapa chini

MWAKA
KUPIMA AFYA
KAGUZI ZA
KAWAIDA
KAGUZI
MAALUM
2001-2005

23,864
26,000
9,612
2006-2010
44,463
22,234
 50,979
JUMLA
68,327
31,846
76,979

Kutokana na kaguzi hizo, wakala umeweza kubaini baadhi ya waajiri ambao
Hawatoi taarifa za ajari zinapotokea na ambao hawasajili sehemu za kazi na
Kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na wengine
Kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa hatua zaidi.

Akizungumza na Tanzania daima Afisa mmoja wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi Mkoani Mwanza ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama ameliambia Tanzania daima kuwa ni kweli upo uzembe uliobainika katika Kiwanda cha Sayona katika kipindi cha mwaka 2012 ambapo  Kiwanda cha Sayona kimetozwa faini mara mbili mfurulizo kutokana na uzembe na huduma duni katika masuala ya Usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi wake.

HAWA NDIYO MOJA WA MAJERUHI WA KIWANDA CHA SAYONA JIJINI MWANZA WAKIHANGAIKA NA VIDONDA
BAADA YA KULIPUKIWA NA JIKO LA KUYEYUSHIA VYUMA KATIKA KIWANDA CHA HICHO.



 Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona LUCAS LUBINZA akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona  kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO
 
 Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona Lucas Nkalango akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona  kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO



  Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona LUCAS LUBINZA akiwa ameumia vibaya sehemu ya nyuma baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona  kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO


 Kwa upande wa nyuma anavyoonekana Lubinza akiwa ameungua vibaya


Saturday, April 6, 2013

Abuse by Police and wife



Abuse by Police and wife






Inbox

x






Description: https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/profile_mask2.png
Present kalalu Kinyala <kinyalapresentkalalu@yahoo.com
11:49 am (1day ago)
Description: https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif

Description: https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif
Description: https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif
Description: https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif
  
Nimebahatika kwa jinsi ya bahati tuu kugundua uwepo wa chama kinachotetea wanaume wanaofanyiwa vitendo vya aibu na wake zao.

 Kwa bahati mbaya zaidi jamii yetu imekuwa na kawaida ya kuwasikiliza wanawake zaidi na kudhani ni wanyonge na hawawezi kufanya ukatili.

Ukatili niliofanyiwa ni kama ifuatavyo. Mwaka wa 2010 mwezi wa nane tarehe mbili askari wa kituo cha tumbi walikuja kwenye kituo cha Kobili Picha ya ndege pamoja na mke wangu wakakamata gari kubwa la biashara ambalo nilikua nimepaki hapo wakaondoka nalo wakidai lilikua gari la wizi.

 Nimekua nikiwadai Polisi hili gari tokea muda huo nimefuatilia hadi ngazi za juu za Polisi hakuna anayeweza kuniambia kwanini walishika gari langu. Nimewaandikia barua ya notice wamekaa kimya, Nimewaona ana kwa ana waishia kudai wanachunguza tukio.
Ni mwaka wa tatu sasa sina kazi sina jinsi ya kupata kipato nje ya hilo gari ambalo lilikuwa ni ajira yangu,Uchunguzi wangu umenipelekea kwenye ukweli kwamba nilifanyiwa kitendo cha ujambazi na Polisi.
Kuna jinsi wanashindwa kumchukulia hatua huyu Polisi aliyefanya huu ujambazi. Pengine kuna shinikizo kutoka nisipopajua. Kama kweli hili gari lilikua la wizi ni mwaka wa tatu sasa kwanini hawamtaki mwizi wampeleke kwenye vyombo vya sheria. 

Nina vielelezo vya kutosha nina omba msaada wenu.

 Ninaitwa Present Kalalu Kinyala


Description: https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gifReply

Description: https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gifForward




Hii imetumwa kwetu na mwenye Email iliyoko hapo juu tuifanyie kazi kama TAMRA

Saturday, February 9, 2013

ALIYEPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI AKATWA MGUU

ALIYEPIGWA RISASI NA ASKARI  POLISI  AKATWA MGUU       
 Na  Antony Sollo  -  Kishapu.
 09/02/2013

HALI si shwari katika mgodi wa mwadui,wananchi wamezidi kuuawa na kujeruhiwa kwa risasi huku Serikali ikiwa haina majibu kuhusu kashfa zinazotokea katika  mgodi huo jambo ambalo hadio sasa wananchi wana mpango wa kuvamia mgodi huo kwa lengo la kuharibu mali za mgodi huo.
Kufuatia hali hiyo,wananchi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mgodi huo wanajipanga kufanya vurugu kubwa katika mgodi huo ili kulipiza kisasi kufuatia kushambuliwa kwa vijana watano ambao waliingia mgodini humo hivi karibuni kama ilivyoripotiwa na Tanzania daima na hatimaye kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao huku mmoja wa vijana hao bwana Geroge Joseph akikatwa mguu.

Hali hii ni mwendelezo wa taarifa nyingi za kuuawa na kujeruhiwa kwa raia  lakini hakuna ufuatiliaji wowote kutoka kwa viongozi wa Serikali hususani vyombo vya ulinzi na usalama kama jeshi la polisi jambo ambalo kwa siku chache zijazo kama hali hii haitarekebishwa watanzania tukashuhudia mapigano makubwa kati ya walinzi wa mgodi na wananchi.

Matukio haya yamegubikwa na usiri mkubwa huku Viongozi mbalimbali wakiendelea kutupiana mpira na kushindwa kueleza bayana juu ya ukweli wa matukio haya na kibaya zaidi majeruhi aliyepata ulemavu huo bwana George Joseph akiwatuhumu viongozi hao akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kwa kushindwa kufika kwa muda muafaka kumuona na kumuombea ruhusa kwa uongozi wa mgodi ili aende kupata matibabu.
Hali hii inatokana na kwamba mgonjwa majeruhi huyo alikuwa akishikiliwa na uongozi wa mgodi huo kwa tuhuma za kuingia mgodini isivyo halali jambo lililosababisha kumchelewesha kwenda kupata matibabu hivyo kuharibika kwa mguu wake na hatimaye kukatwa.

Kijana huyo alilazwa katika hospitali ya mgodi wa mwadui tangu tarehe 9/01/2013 huku akiwa chini ya ulinzi wa askari wa mgodi huo lakini kukiwa hakuna huduma zilizokuwa zikitolewa jambo lililosababisha aombe kupewa rufaa bila mafanikio ambapo na hatimaye ndugu walifanikiwa kumuondoa hospitalini hapo kwa kutumia nguvu na kumpeleka hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza ambako amelazwa hadi sasa.

Akilalamikia viongozi wa Serikali mgonjwa huyo Bwana George Joseph anasema”ndugu mwandishi,Mkuu wa Wilaya ya Kishapu ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya alikuwa ni mtu wa kwanza kumjulisha juu ya tukio hili na aliahidi kufika hospitalini lakini hakufanya hivyo hadi sasa nimethirika na kuwa mlemavu kwa kukatwa mguu wangu.

Kuhusu kauli ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kuwa hana taarifa,inashangaza na inasikitisha sana kwani askari waliokuwa wamekuja hapa kwa ajili ya kufanya operesheni walitoka mkoani Shinyanga.

Askari waliofika  kunichukua maelezo nao pia walitoka ofisi ya upelelezi ya Mkoa wa Shinyanga hata operesheni hii huandaliwa na Mkoa,je haya madai kwamba hana na taarifa yana lengo gani kama si kuficha ukweli wa jambo hili? na anafanya hivyo kwa faida ya nani amehoji bwana George.

Wakiongea na Tanzania daima wananchi waliozungumzia tukio hili walisema ndugu mwandishi, kwa kweli kuna idadi kubwa sana ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika mgodi huu lakini hatuoni viongozi wetu wakifuatilia masuala haya sijui hawana uchungu na wananchi ambao ndiyo rasrimali ya taifa hili.
Kwa sasa tukio hili limetupa hofu kubwa na sasa tunaiomba Serikali ijiandae kuona machafuko makubwa kwa vile tumechoshwa na vitendo hivi katika maeneo yetu.

tuna mpango wa kwenda kuvamia mgodi na kuchoma ofisi mbalimbali pamoja na kufanya uharibifu mkubwaili kuibua na kuweka wazi manyanyaso tunayofanyiwa na mawekezaji wa mgodi wa Williamson mwadui maana kuna usiri mkubwa mno kuhusu matukio ya unyanyasaji wa wananchi wa Maganzo na vitongoji vyake. 

Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea Ofisi za SHILEMA zilizopo katika mji mdogo wa Maganzo, Katibu Msaidizi wa SHILEMA bwana Hamza Yusuph amesema watu wengi wamepoteza maisha na viungo vyao kwa sababu ya kuingia mgodini mwadui pasipo na uhalali wa kuingia mgodini humo,wote tunajua kuwa kuingia mgodini ni kosa la jinai,lakini pia  hatua za watendaji wa jeshi la Polisi  kujichukulia sheria mkononi zinatokana sheria na mamlaka ipi?

 Kwa nini watu hawa wasikamatwe na kufikishwa mbele ya sheria kuliko kufanya ukiukwaji huu wa sheria na kusababisha wimbi la vijana walemavu kuongezeka! Vitendo hivi havikubaliki kabisa alisema bwana Selemani mkaji wa kitongoji cha majimaji mji mdogo wa Maganzo.

Bwana Yusuph amewalalamikia pia viongozi wa kisiasa wanaotumia mwavuli wa kisiasa katika masuala yanayohusu maisha ya watu ili kujijengea umaarufu katika nyakati za uchaguzi huku akiwalaumu viongozi wa kamati ya mzunguko wa mwadui kwa kujali masilahi yao  binafsi na kusahau kwamba wao ni wawakilishi wa wananchi.
Akizungumzia fedha zinazotolewa mgodini hapo bwana Yusuph amesema haelewi kama fedha hizo zinatolewa kama zawadi  au ni wajibu wa kampuni katika kuihudumia jamii hususani huduma za msingi kama Elimu,Afya,Miundo mbinu,Maji,Umeme naBarabara kama ilivyo katika maeneo mengine.

Bwana Yusuph amelaumu pia Serikali kwa kushindwa kuweka wazi mikataba ya Makampuni ya uchimbaji wa madini nchini kwa kuwa wananchi hadi sasa hawaelewi mambo mbalimbali zikiwemo haki zao dhidi ya makampuni ya uwekezaji katika maeneo yao.
Tanzania daima ilibisha hodi katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bwana Justine Sheka na kufanya mahojiano naye ambapo alianza kwa kusema,ndugu mwandishi,sisi kama viongozi wa Serikali Wilayani Kishapu tunashangazwa na uongozi wa mgodi wa Mwadui kwa kuendesha shughuli zake kwa ubabe na usiri katika mapato yanayotokana na mgodi huo.
Hadi sasa uingiaji ndani ya mgodi huo una urasimu mkubwa kiasi kwamba hata Mbunge wa Jimbo anapohitaji kuingia na kuangalia utendaji wa shughuli za mgodi huo zinavyofanyika ni shida,unaingia ukiwa chini ya ulinzi mkali na mara nyingine yapo madai kuwa ni lazima utoe taarifa mapema kwa uongozi wa mgodi.
Lakini pia amesikitishwa na jinsi Serikali ilivyofanya siri kuhusu uwakilishi wake katika kukagua uzalishaji wa madini na namna ya kupata taarifa mbalimbali ili kuweza kuona kama kweli mali inayopatikana ndiyo inayotolewa taarifa  kama ilivyo katika maeneo mengine yaliyo na migodi.

Inasemekana ni muda mrefu mgodi wa Mwadui umekuwa ukiendesha shughuli za uchimbaji wa madini Wilayani Kishapu bila kuwa na mwakilishi wa Serikali ambaye anafanya ukaguzi jambo linalohofiwa kuporwa kwa madini na kuisababishia Hasara Serikali.
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga bwana Evarist Mangala alipotafutwa kujibu malalamiko juu ya tuhuma zinazotolewa na mgonjwa aliyekatwa mguu bwana George Joseph alisisitiza kwamba bado hana taarifa lakini akashauri kwamba mgonjwa aandike barua ya malalamiko juu ya tukio hilo ili aweze kulifanyia kazi.
                            
                           Mwandishi 0787 565 533
                          Email:antonyjilala@yahoo.com

Hapa ndipo ilipo hospitali ya bugando alipolazwa Bwana George na hatimaye kukatwa mguu wake  Picha na Antony Sollo


Bwana George Joseph Bwisige akiwa amekatwa mguu wake katika Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza .
                                                          Picha na Antony Sollo