Sunday, December 30, 2012

UKATILI WA KUTISHA
KUELEKEA MWAKA MPYA 2013
WANAUME WAWILI WAUNGUZWA VIBAYA  JIJINI DAR ES SALAAM.
Katika kuelekea kufunga mwaka 2013,wanaume wawili jijini Dar Es salaam wamejikuta katika mazingira magumu baada ya kupata majeraha makubwa  hii ni baada ya kumwagiwa mafuta yaliyokuwa jikoni kwa ajili ya ugomvi wa mapenzi.
Mmoja wa majeruhi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa ajili ya aibu aliyo nayo ambaye ni mkazi wa Kibanda cha Mkaa jijini Dar Es salaam alikutwa na mkasa huo siku ya tarehe 29 akiwa amelala nyumbani kwake ambapo alimwagiwa mafuta yaliyokuwa yamechemshwa na mke wake kwa ajili ya kupikia maandazi hali iliyopelekea kuungua vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.
Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Wilayani Kibaha Mkoani pwani na hali yake ni mbaya lakini waganga wamejitahidi kwa kiwango cha hali ya juu kumnusuru maisha yake ambapo baada ya Kutembelewa na Katibu Mkuu wa TAMRA bwana Antony Sollo alikataa katakata kupigwa picha hali iliyoashiria kuwa huenda kosa lilikuwa ni la kwake,hivyo kupelekea kuona aibu kulitolea ufafanuzi tatizo hilo.
Majeruhi wa pili ni Bwana Method Msabila mkaaji wa mbezi mtaa wa Konoike  Road ambae ni mfanyabiashara umri wa miaka 35 anaeleza kuwa siku ya tukio Msabila aliagiza chakula kwa mama ntilie ambaye alikuwa akifanya biashara ya kupika chakula jirani na duka la majeruhi huyo.
Akieleza kwa huzuni kubwa kufuatia kuungua vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake bwana msabia amesema kuwa aliagiza chakula kwa lakini alikaa muda mrefu bila kupelekewa chakula hicho ambapo aliamua kwenda kuangalia kwa nini chakula hicho kilikuwa hakijaletwa.
Alipofika katika hoteli hiyo aliuliza kwa nini chakula kimechelewa ambapo baada ya kuambiwa kuwa chakula kilikuwa kimekwisha Jibu hilo lilikasirisha bwana Msabila kufuatia kusubiri chakula hicho kwa muda mrefu na baada ya kujibizana ukatokea mzozo uliopelekea kutoelewana baina ya mama huyo aliyejulikama kwa jina moja la Amina ambapo walitukanana na baadaye bwana Msabila alirudi katika eneo lake la kazi na baada ya kukaa na kujisahau ambapo nbaada ya muda alishangaa kumuona Amina akija pale na sufuria ambalo lilikuwa na maji na baada ya muda mfupi mno kupita ,Amina alimmwagia maji ya moto na kuungua vibaya bwana Msabila na haraka haraka mama huyo alikwenda kiyuo cha polisi cha Mbezi kwa Yusuf na kufungua taarifa ya uongo kwamba amefanyiwa fujo na majeruhi huyo
Baada ya muda bwana Msabila alichukuliwa na wasamalia wema  na kupelekwa kituo cha polisi ambapo Askari aliyempokea kwa maelezo ya bwana Msabila alimwambia kuwa wewe ni mtuhumiwa umefanya fujo hivyo alimpatia PF3 ili aende kupata matibabu na baadaye aje afunguliwe mashtaka kufanya fujo.
Katibu Mkuu wa TAMRA Bwana Antony Sollo alipata taarifa na kuamua kwenda Hospitali ya Tumbi alipofika hospitalini hapo alishuhudia mwili wa bwana Msabila ulivyoungua vibaya  na maji ya moto ambapo alimpa pole na kuahidi kufuatilia suala hilo katika kituo cha polisi Mbezi kwa Yusufu
Akiwa njiani kuelekea mbezi alipigiwa simu na kujulishwa kuwa mtuhumiwa Amina tayari amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo alipofika kituoni hapo alimuona mtuhumiwa huyo na baada ya kumhoji hakuwa na la kusema na zaidi ya yote kujuta kwa kuchukua maamuzi mabaya kiasi hicho kwa kummwagia maji ya moto Bwana Msabila ambapo mtuhumiwa huyo amefunguliwa kesi ambapo namba ya kesi hiyo ni KMR/RB/157661/2012 kosa la kujeruhi.
Hali hii inathibitisha kuwa wapo kina mama wababe kuliko hata wanaume na hali hii ya kutokuwa na taarifa za ukiukwaji huu wa haki dhidi ya mwanaume ni kutokana na kutokuwa na chombo cha kuratibu matukio mbalimbali ambapo anapenda kuifahamisha jamii kuwepo kwa matukio ya ukiukwaji wa Haki yanayofanywa na wanawake .
 Katibu Mkuu wa TAMRA amelaani vikali ukatili uliofanywa na wanawake  na wanaume na kuwataka wananchi kuripoti matukio haya pindi yanapotokea ili kuwezesha kuwa na takwimu mbalimbali sahihi kuhusu ukatili unaofanywa na wanawake pia badala ya kuwa na takwimu za upande mmoja  wa wanaume,na ameitaka jamii ya Watanzania hususani wanaume kote Nchini kujitokeza katika kutoa taarifa za ukiukwaji wa Haki za Binadamu na ukatili kama huu bila woga maana hakuna mtu atakayewazomea kwani hii pia ni hali ya kwaida katika kupashana habari.

 Hapa ni Kibao cha Hospitali ya Tumbi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani


 Bwana Methody Msabila mwenye Pamba kifuani akiwa ametulia baada ya maongezi yake na Katibu Mkuu wa TAMRA hayupo pichani baada ya kutembelewa Hospitalini kujua hali yake.



Bwana Methody Msabila mwenye Pamba kifuani akiwa na wagonjwa wenzake katika Hospitali ya Tumbi

TAMRA itaendelea kuwapa taarifa mbalimbali kupitia blog yake ya www.tamratanzania.blogspot.com hivyo karibuni kila wakati muweze kuangalia matukio mbalimbali.
ASANTENI SANA NA POLENI KWA TAARIFA YA KUSIKITISHA.
UONGOZI WA TAMRA UNAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2013

Saturday, December 29, 2012

The theme for International Men’s Day 2012


The theme for International Men’s Day 2012 (Monday 19th November) has been announced.
This year the theme of the international day of observance will be Helping Men and Boys Live Longer, Happier, Healthier Lives.
In the build up to the event, supporters of the day are being asked to focus on five key challenges linked to health and wellbeing which are:
1. Improving men’s life expectancy
2. Helping men get help
3. Improving boys’ education
4. Tackling tolerance of violence against men and boys
5. Promoting fathers and male role models
The Men’s Network in Brighton & Hove will be the UK lead co-ordinator for International Men’s Day in 2012. For more information on this year’s theme then click here now to  visit the International Men’s Day UK Website.
HELPING MEN AND BOYS LIVE LONGER, HAPPIER, HEALTHIER LIVES
International Men’s Day in the UK on Monday 19th November 2012 is all about giving men and women an opportunity to:
·         Have some serious fun
·         Highlight some serious issues
·         Celebrate Britain’s men and boys in all their hairy diversity
To help bring some focus to the serious side of International Men’s Day, each year we choose an annual theme that help supporters all over the world to focus our collective minds on  an issue of global significance.
In the run up to International Men’s Day 2012 (Monday 19th November) we’re asking supporters of the day to focus on five key challenges that will help us improve the health and wellbeing of men and boys all over the world.
Some of the universal health issues that men and boys in all countries around the globe face include lower life expectancy, difficulty accessing mental health services, educational disadvantages, lack of male role models and tolerance of violence against men and boys.
To help us focus our collective minds upon helping men and boys live longer, happier, healthier lives, the five key challenges that the International Men’s Day team is inviting men and women all over the world to address are:
1. IMPROVING MEN’S LIFE EXPECTANCY:
From the moment a boy is born he can expect to live a shorter life than his female counterparts in all but four countries on the planet. There is also a huge gap in life expectancy between rich and poor countries with men in Mozambique reaching an average age of 38 while in Iceland, Israel and Switzerland men live twice as long until the age of 80. There are also huge gaps in life expectancy within countries, with men born in the poorest parts of the United Kingdom, for example, dying 10 years sooner than their fellow countrymen in the wealthiest parts of the capital city. Boys are not genetically programmed to die young so our first challenge this International Men’s Day is to ask countries taking part to consider how we can help all men and boys live longer, happier, healthier lives – no matter how poor they are and no matter what country they are born in.
2. HELPING MEN GET HELP:
Every year poor mental health drives over three quarters of a million people to commit suicide – and around two thirds of them are males. Men and boys all over the world can find it more difficult to access help for mental and emotional health problems and most prison populations include a significant number of men with mental health issues. This International Men’s Day we are asking participating countries to consider how we can help more men and boys get the help and support they need and to take action on behalf of the hundreds of thousands of men who will take their own lives this year.
3. IMPROVING BOYS’ EDUCATION:
Poor education is linked to poor health outcomes later in life so improving boys’ education will also help men and boys live longer, happier healthier lives. This International Men’s Day we are asking people to explore why boys in richer countries are underperforming girls and also less likely to be in education, and why tens of millions of boys in poorer countries are still not completing a primary education? How can we address truancy and poor literacy rates which leave boys prone to adult unemployment, substance abuse, obesity, depression and poverty? What action can we take to focus on boys’ education in a way that closes the gap between girls and boys, addresses the gaps between rich boys and poor boys, and helps us to improve the long-term health and wellbeing of all men and boys.
4. TACKLING TOLERANCE OF VIOLENCE AGAINST MEN AND BOYS:
Violence has a major impact on men’s health all over the world. Every year over half a million people die from violence and 83% of them are men and boys. The same proportion of the global burden of disease (ill-health, disability or early death) from violence is borne by boys and men.Yet while there are now a number of deserved global campaigns to tackle violence against women and girls, there are no such campaigns to help men and boys. Why are we so tolerant of violence and abuse against boys and men and why do we still tolerate a world where we send boys and young men to fight wars on behalf of the adults in power? This International Men’s Day we are asking for actions we can take to help men and boys live in a less violent world and challenge our collective global tolerance of violence against men and boys.
5: PROMOTING FATHERS AND MALE ROLE MODELS
Fathers and male role models play a vital role in helping boys make a healthy, happy and positive transition from boyhood to manhood. How can we give boys a right to family life that gives them an equal opportunity to know and experience both their father and mother and ensure that their role as a future father is equal to girls’ role as future mothers? Giving boys a range of positive life choices in terms of family, work and leisure can help us reduce the number of boys whose choices are limited and end up poor, illiterate, unemployed, homeless, imprisoned and isolated. This International Men’s Day we are asking what actions we can take to give all boys access to a variety of male role models and ensure their country’s laws and practices give them an equal right to fatherhood, with all the support they need to be the best fathers they can be.
Addressing each of these challenges will help us to help men and boys all over the world to live longer, happier, healthier lives, which is why we are inviting supporters of International Men’s Day to join us in taking on one of more of these five key challenges in 2012.

Viongozi wa TAMRA TAIFA wakiongea na waandishi wa Habari kituo cha East Africa Radio walipokuwa wamealikwa kwa ajili ya kutambulisha masuala mbalimbali yanayohusu matatizo ya wanaume nchini.
We  wishes A New year  2013
ANTONY  SOLLO
GENERAL SECRETARY FOR TAMRA TANZANIA

Friday, December 28, 2012


TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION
CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA

”TAMRA”
Equal treatments for all

UTANGULIZI

TAMRA ni Asasi ya kiraia iliyoanzishwa na wanaume wa Tanzania kwa lengo la kutoa msaada wa Kisheria pamoja na Elimu ya Haki na Wajibu katika mahusiano ya kindoa kati ya mwanamke na mwanaume.
Kuanzishwa kwa asasi hii kumekuja katika kipindi hiki baada ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa wapo wanaume  wengi wanaofanyiwa vitendo vya ukatili katika masuala ya ndoa kwa kunyimwa haki zao za kindoa kutupiwa virago pindi mwanamke anapoamua kumchoka mwanamme kufuatana na kukosa kipato, kupungukiwa nguvu za kiume na mambo kama hayo , jambo ambalo limeonekana kuwa ni chanzo cha migogoro katika ndoa inayosababisha ongezeko la watoto wanaoishi bila wazazi wa pande zote mbili yaani  [ Baba na Mama] huku hali hii ikiigharimu jamii na wanandoa kupigana na kusababisha majeraha na mauaji katika jamii.

Si hivyo tu Mwanamme wa Tanzania amekuwa ni mvumilivu kwa vile amekuwa akitendewa mambo yote haya bila kuwa na chombo cha kukemea vitendo hivi jambo lililotoa ushawishi kwa waanzilishi wa chama hiki kupata uchungu na hatimaye kuamua kuanzisha Asasi hii.

Muda mrefu mwanaume wa Tanzania hakupata wapi  pa kwenda kupata msaada wa kisheria, imefika wakati wanaume kuwa na  chama cha kuwatetea dhidi ya unyanyasaji kutoka kwa wake zao katika nyanja mbali mbali ikiwemo mambo ya ndoa,urithi wa mali kwa wagane, pamoja na ulezi wa watoto.

TAMRA kinaenda mbali katika kuelimisha wanaume juu ya haki zao za msingi pamoja na kuwaelimisha juu ya wajibu wao kama baba katika kuitunza familia yake,kuondoa mfumo dume na mfumo jike, kupiga vita unyanyasaji kwa mke na watoto,urithi wa mali kwa wajane na wagane pamoja na kulea watoto kabla na baada ya kufariki kwa wanandoa.
Jina la asasi: Asasi hii itajulikana kuwa ni Chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania/Tanzania Men’s Rights Association kwa kifupi TAMRA

(1) Kuanzishwa kwa TAMRA:
Asasi  ya TAMRA ilianzishwa 01/05/2012

(2) Makao Makuu.
Makao makuu ya TAMRA yatakuwa katika Mtaa wa Mpakani ‘A”Kijito Nyama Jijini Dar Es Salaam kituo cha Afrika sana Nyumba Block namba 45.
                    
vile vile kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Jijini MWANZA

(3)  Anuani ya Chama ni. Chama Cha Kutetea Haki za Wanaume Tanzania.
    S.L.P 60065
   Dar Es Salaam - Tanzania
    Simu: Mwenyekiti TAMRA TAIFA +255 784 203 556
             Katibu Mkuu TAMRA TAIFA +255 787 565 533
    Baruapepe:tamratanzania@gmail.com
    Blog:   yetu ni  www.tamratanzania.blogspot.com

TAFSIRI
“TAMRA” itamaanisha ni TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION.
       KUTAKUWA NA VIONGOZI WAFUATAO WA TAMRA
·         Kutakuwa na Mwenyekiti wa TAMRA Taifa.
·         Katibu mkuu wa TAMRA Taifa.
·         Mweka Hazina wa TAMRA Taifa.
·         Katibu wa Uhamasishaji wa TAMRA Taifa.
·         Wajumbe wa Bodi ya TAMRA 

KAZI ZA TAMRA.
TAMRA itakuwa na kazi zifuafuatazo:
(1)  Kutetea wanaume dhidi ya unyanyaswaji katika ndoa.
(2) Kutoa elimu juu haki za Wanamme
(3) Kuwaelimisha wanamme kuondokana na mfumo dume/jike.
(4) Kuelimisha wanaume kuhusu haki na usawa kati ya mwanamme na  mwanamke katika kutoa maamuzi kwa mambo mbalimbali ya kifamilia, kisiasa na kiuchumi.
(5) Umiliki wa mali katika familia.
(6) Haki ya kushiriki na kufurahia ndoa.
(7) Kuelimisha jamii juu ya Haki ya kumiliki mali kwa pamoja kabla na baada ya kifo cha mmoja wa wanandoa.
(8) Kuelimisha wanandoa kuhusu Haki na wajibu wa kuheshimiwa na kupendwa kwa kila  mwanandoa kama ilivyo katika maandiko matakatifu bila kuathiri itikadi za dini.
(9) Kuhakikisha kwamba TAMRA inashirikiana na  taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuondoa imani potofu dhidi ya mwanamme ili kujenga mahusiano mazuri katika familia badala ya kuchochea uhasama kwa kumkandamiza mwanamme kuwa ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya familia.
10.kuhakikisha kuwa kuna usawa na uhuru wa kujieleza pindi mashauri ya ndoa yanapopelekwa katika vituo vya Polisi kwa uchunguzi na hatimaye hatua ya kupelekwa  katika vyombo vya maamuzi.
11.Kuhakikisha kuwa wapo Mawakili wa kutosha panapotokea mashauri katika Mahakama watakaotetea Haki za Wanaume   ili kuhakikisha Haki inatendeka

MALENGO YA TAMRA.

TAMRA itakuwa na malengo kama ifuatavyo:-
(1)  Kupigania Haki za mwanaume katika masuala mbalimbali ikiwamemo kulinda na kudumisha ndoa.
(2) Kulinda Haki ya mwanaume ngazi ya familia ,kitaifa na kimataifa.
(3) Kuelimisha waathirika wa unyanyasaji
(4) Kutoa msaada wa kisheria Bure kwa kutumia mawakili wa TAMRA.
(5) Kutoa elimu ya Afya na malezi ya mtoto wa kiume ili akue katika maadili yanayozingatia haki sawa kwa wote kuondoa dhana ya mfumo dume.
(6) Kutoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa yasiyokuwa na tiba ikiwamo Ukimwi (HIV/AIDS).
(7) Kutoa elimu na mafunzo kwa wanamme ili kuwafundisha ujasiria mali kuondoa  utegemezi .
(8) Kufanya upatanishi na usuluhishi kwa wanandoa kwa kuzingatia mila,Desturi,Dini pamoja na sheria za Nchi.
(9) Kutoa elimu kwa wanaume kukubali mabadiliko ya mwili kufuatana na umri kuwa mkubwa kati ya mwanamme na mwanamke.
10   Kulinda Haki za kila raia bila kujali itikadi za dini, rangi, kabila jinsia na taifa.
      11  Kutoa Elimu ya uraia.
11    Kushirikiana na serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa katika maadhimisho ya  siku ya mwanamme Duniani ikiwemo kuandaa sherehe  hizo kitaifa kufuatana na kalenda ya kimataifa kila mwaka.
12   Kutoa misaada kwa makundi ya wasiojiweza  yatima, wazee,wagonjwa ,wakimbizi majeruhi wa ajari, majanga kama njaa,mafuriko, shule au kujenga majengo ya kutoa huduma za afya na elimu kulinda na kutunza mazingira kuangalia chaguzi ndani na nje ya Tanzania.
  
 VIONGOZI WA TAMRA KATIKA PICHA  

 KATIBU WA UHAMASISHAJI WA TAMRA TAIFA BWANA HATIBU MGEJA AKIWA NA MWEKA HAZINA WA TAMRA TAIFA BWANA JUMA KOMBO WAKIWA KATIKA STUDIO ZA EAST AFRICA RADIO JIJINI DAR ES SALAAM
MWEZI JUNE 2012.


KATIBU MKUU WA TAMRA TAIFA BWANA ANTONY SOLLO  AKIFURAHIA JAMBO WAKIWA NA KATIBU WA UHAMASISHAJI WA TAMRA TAIFA BWANA HATIBU MGEJA KATIKA STUDIO ZA EAST AFRICA RADIO JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 2012

TAMRA INAWATAKIA HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2013 KARIBUNI KWA MCHANGO WA MAWAZO,USHAURI

BELENSI ALKADI - MWENYEKITI WA TAMRA TAIFA   0784203556
ANTONY SOLLO - KATIBU MKUU WA TAMRA TAIFA 0787565533


  















Tuesday, December 25, 2012

Our theme in 2012 | Positive Male Role Models


TAMRA TANZANIA

Our theme in 2012   | Positive Male Role Models
 Objectives of International Men's Day include a focus on men's and boy's health, improving gender relations, promoting gender equality, and highlighting positive male role models. It is an occasion for men to celebrate their achievements and contributions, in particular their contributions to community, family, marriage, and child care while highlighting the discrimination against them.
The November IMD is a significant date as it interfaces the popular 'November' charity event and also with Universal Children's Day on Nov 20 with which IMD forms a 48 hour celebration of men and children respectively, and of the special relationships they share.
The ability to sacrifice your needs on behalf of others is fundamental to manhood, as is honour. Manhood rites of passage the world over recognise the importance of sacrifice in the development of Manhood.
Men make sacrifices everyday in their place of work, in their role as husbands and fathers, for their families, for their friends, for their communities and for their nation. International Men's Day is an opportunity for people everywhere of goodwill to appreciate and celebrate the men in their lives and the contribution they make to society for the greater good of all.
Methods of commemorating International Men's Day have included public seminars, conferences, festivals and fundraisers, classroom activities at schools, radio and television programs, Church observances, and peaceful displays and marches. The manner of observing this annual day is optional; any organizations are welcome to host their own events and any appropriate forums can be used.  This year the theme is Positive Male Role Models. Should you want to choose another theme for your particular celebration you are quite at liberty to do so.
 International Men's Day is celebrated in over 60 countries of the world. Too many to list. Join us on November 19 2013 in celebrating the contribution men and boys make to those around them, to their family and friends, their work place and the community, the nations and the world.
Dads 4 Kids is honoured to host the Men's Day we invite you to join the global celebrations.
Antony J Sollo
General Secretary for TAMRA TANZANIA  +255 787 565 533
Merry XMAS &Happy New year 2013

TAMRA YAONYA

  
TAMRA YAONYA WANAUME WAZINGATIE SHERIA ZA NCHI VINGINEVYO WANAUME WAKOROFI HAITAWASAIDIA
Na - SELEMANI PHARLES MABALA - DAR ES SALAAM
Chama cha kutetea haki za Wanaume Tanzania TAMRA kimewataka Wanaume kote nchini kuzingatia sheria za nchi na kuacha mara moja kuonyesha ubabe kwa kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wanawake wakati wakiwa wametenda makosa mbalimbali majumbani mwao vinginevyo hakitakuwa tayari kumlinda mwanaume yeyote ambaye atakuwa amekwenda kinyume na matakwa ya chama hicho.
Kauli hiyo imetolewa na viongozi wa chama hicho nchini akiwemo mwenyekiti wa chama hicho nchini Bwana Belensi Alkadi na  Katibu Mkuu wa chama hicho nchini Bwana Antony Sollo walipokuwa wakizungumzia hoja mbalimbali pamoja na changamoto zinazowakabili wanaume mbalimbali nchini.
Bwana Sollo amesema wanaume hukumbana na matatizo makubwa katika familia zao lakini hakuna namna nyingine itakayosaidia kuidumisha amani ndani ya familia hizi isipokuwa wanahitaji kuwa wavumilivu,na zaidi ya yote watumie busara zaidi,hekima zaidi katika kuyamaliza masuala mbalimbali na changamoto za wanandoa kwa vile hakuna kitu kinachomkuta mwanandoa kwa bahati mbaya bali hatua ya kwanza ni kukumbuka kuwa wanandoa hawa waliapa viapo vya utii kwa mungu wao siku ya ndoa yao viapo hivi vinakwenda sambamba na uvumilivu katika mambo mbalimbali ikiwemo umaskini,utajiri, magonjwa na mambo mengine ya aina hiyo ambapo bwana Sollo ameshangazwa na tabia ya mmoja wa wanandoa kufikia kumlalamikia mwenzake kuwa ameshindwa kuvumilia shida za mwenzake na kwa sasa hana uwezo tena wa kuendelea kuishi na mtu ambaye hawezi kumtunza na kuamua kuivunja ndoa bila ya kuwashirikisha hata viongozi wa dini pamoja nan wazazi ambao ni mojawapo wa waliobariki na kutoa kibali cha wawili hawa kuishi kama mme na mke.
Naye Mwnyekiti wa chama hicho nchini akizungumzia hali ya mifarakano ya kifamilia amesema kuwa moja ya vitu vinavyochangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa matatizo katika ndoa na kupelekea kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani ni pamoja na mmomonyoko wa maadili ya Mtanzania kwa vile baadhi ya familia zimekuwa na majukumu ya kujitafutia maisha huku zikiwaachia watumishi kulea watoto bila kushiriki kwa wazazi kufundisha malezi bora kwa watoto,maendeleo ya Sayansi na teknolojia kwa vile kwa sasa watoto hujua haraka mambo makubwa ambayo umri ulikuwa haujafikia kuyajua na kuyatenda  jambo linalosababisha kupungua kwa kasi kubwa kwa heshima katika jamii.
 Akizungumzia malezi na makuzi ya kipindi kilichopita Bwana Sollo amesema kuwa zamani watu walikuwa hawawezi kuzungumza juu ya mambo ya mahusiano ya kindoa tofauti na ilivyo sasa ambapo tafiti zinaonyesha kuwa watoto wengi kuanzia shule za msingi na sekondari huanza mahusiano ya kimapenzi mapema na matokeo yake kushusha kiwango cha Elimu kwa kuwa mapenzi na shule ni sawa na kulima huku ukishindwa kupalilia na hatimaye kwa sababu ya kujitetea tu mtu anasema kuwa kuna uchawi umefanyika na kupelekea kushindwa kwake kuvuna mazao.
Hata hivyo akizungumzia changamoto walizo nazo wanandoa hasa wa kiume ni juu ya umaskini na hata kipato, kwa vile kwa sasa baadhi ya wanaume wamekuwa wakipambana na matatizo makubwa baada ya kushindwa kumudu maisha kufuatana na changamoto zinazowakabili ikiwamo kukosa kipato, ugonjwa sugu kama mabusha matende,Ukimwi HIV/AIDS na mambo mengine kama hayo.
TAMRA Imejipanga kukabiliana na changamoto hizi kwa kutoa elimu kwa mwanaume wa Tanzania pamoja na mototo kiume ili kuondoa dhana ya mfumo dume katika kuweka haki sawa kwa wote,amewaomba wanaume kuwa na subira na kuacha kujichukuliasheria mkononi kwa vile endapo watatenda mambo yaliyo kinyume na malengo ya chama hiki hawatakuwa tayari kuwatetea wanaume ambao watakiuka haki za binadamu kwa vile watakuwa wamevunja kanuni taratibu sheria pamoja na katiba inayoongoza nchi.
Nikweli yapo mambo yanayofanyika kwa uonevu lakini TAMRA iko macho sana kulinda na kutetea haki sawa kwa wote kwa vile siku ya Alhamisi wiki hii Katibu mkuu baada ya kuhojiwa na kituo cha ITV aliacha namba za mawasiliano na hatimaye alipigiwa simu kutoka Mkoa wa Geita ambako alipewa taarifa ya mtu mmoja ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa sungusungu kwa masaa kadhaa akisubiri kusurubishwa na alipopata wasaa wa kwenda kujisaidia tu aliomba msaada wa simu na kupata nafasi ya kuongea  na katibu Mkuu wa TAMRA Bwana Antony Sollo ambapo Katibu huyo baada ya kupata maelezo aligundua ukiukwaji wa haki za binadamu na hivyo  aliwaagiza sungusungu hao kumuachia mkara moja Bwana Malimi mkaazi wa Kabuhima Runzewe Mkoani Geita na baada ya hapo walitoa taarifa kuwa tayari Bwana Malimi yuko nje na hivyo suala lake litafikishwa panapohusika.
Akielezea tukio hilo Katibu Mkuu wa TAMRA anasema, ilikuwa saa kumi jioni nilipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa yeye ni Bwana Malimi kutoka kijiji cha Kabuhima  Runzewe Mkoani Geita ambapo yeye alikuwa ameenda kwenye mihangaiko yake tangu asubuhi ,cha kushangaza aliporudi tu alimkuta mke wake amelewa chakali na watoto wake hawajala chakula tangu asubuhi na alipouliza kulikoni akajibiwa kuwa mimi9 siyo House Girl wa familia hiyo na kama anaona vipi aende kutafuta House Girl atakayekuwa mtu wa kuhudumia familia hiyo jambo lililomfanya agadhabike na kumpiga kofi mke wake na baada ya muda mfupi mama huyo alipiga simu mara walitokea watu walikuja na kumkamata Bwana Malimi na kumpeleka ofisi ya sungusungu na kumuweka chini ya ulinzi  ambapo mwenyekiti wa sungusungu aliomba watoe fedha kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yao ambapo mama huyo alitoa shilingi elfu themanini papo kwa papo huku akimuacha hoi mmewe kwa vile alikuwa hajui fedha hizo mkewe alizitoa wapi na hivyo alishinikiza akae rumande hadi siku inayofuata ambapo baada ya kituo cha ITV kurusha moja kwa moja mahojiano na Katibu Mkuu wa chama hicho ndiko kulipelekea ukombozi wa Bwana Malimi na Amewataka wanaume kote nchini kukiunga mkono na kukiamini chama hiki kuwa ni ukombozi wa mwanaume na ni mlinzi wa Haki za Binadamu dhidi ya ukiukwaji wa sheria na kanuni za nchi.
Baadhi ya wananchi wamekipongeza kituo cha ITV kwa kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamiin ya Watanzania nchini kwa kuita watu mbalimbali kituoni hapo ili kuzungumzia masuala mbalimbali ambayo yana faida kwao na wamevitaka vituo vingine viige mfano huu ili Taifa letu liendelee kuidumisha Amani yetu kuiweka nchi katika utulivu na usalama.


Mwenyekiti wa TAMRA Bwana Belensi Alkadi akisikiliza mafunzo ya utetezi wa Haki za Binadamu katika Hotel ya White Sands Resort jijini Dar Es Salaam


 

Katibu Mkuu wa TAMRA Bwana Antony Sollo wa kwanza kushoto akiwa na baadhi ya wanasheria wa Chama cha kutetea Haki za Wanaume katika Hotel ya White Sands Resort Jijini Dar Es Salaam


 
Mwanasheria wa TAMRA Bwana Ben Shebakaki akiwa katika mafunzo ya utetezi wa Haki za Binadamu yaliyofanyika katika Hotel ya White Sands Resort jijini Dar Es Salaam