Sunday, December 30, 2012

UKATILI WA KUTISHA
KUELEKEA MWAKA MPYA 2013
WANAUME WAWILI WAUNGUZWA VIBAYA  JIJINI DAR ES SALAAM.
Katika kuelekea kufunga mwaka 2013,wanaume wawili jijini Dar Es salaam wamejikuta katika mazingira magumu baada ya kupata majeraha makubwa  hii ni baada ya kumwagiwa mafuta yaliyokuwa jikoni kwa ajili ya ugomvi wa mapenzi.
Mmoja wa majeruhi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa ajili ya aibu aliyo nayo ambaye ni mkazi wa Kibanda cha Mkaa jijini Dar Es salaam alikutwa na mkasa huo siku ya tarehe 29 akiwa amelala nyumbani kwake ambapo alimwagiwa mafuta yaliyokuwa yamechemshwa na mke wake kwa ajili ya kupikia maandazi hali iliyopelekea kuungua vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.
Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Wilayani Kibaha Mkoani pwani na hali yake ni mbaya lakini waganga wamejitahidi kwa kiwango cha hali ya juu kumnusuru maisha yake ambapo baada ya Kutembelewa na Katibu Mkuu wa TAMRA bwana Antony Sollo alikataa katakata kupigwa picha hali iliyoashiria kuwa huenda kosa lilikuwa ni la kwake,hivyo kupelekea kuona aibu kulitolea ufafanuzi tatizo hilo.
Majeruhi wa pili ni Bwana Method Msabila mkaaji wa mbezi mtaa wa Konoike  Road ambae ni mfanyabiashara umri wa miaka 35 anaeleza kuwa siku ya tukio Msabila aliagiza chakula kwa mama ntilie ambaye alikuwa akifanya biashara ya kupika chakula jirani na duka la majeruhi huyo.
Akieleza kwa huzuni kubwa kufuatia kuungua vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake bwana msabia amesema kuwa aliagiza chakula kwa lakini alikaa muda mrefu bila kupelekewa chakula hicho ambapo aliamua kwenda kuangalia kwa nini chakula hicho kilikuwa hakijaletwa.
Alipofika katika hoteli hiyo aliuliza kwa nini chakula kimechelewa ambapo baada ya kuambiwa kuwa chakula kilikuwa kimekwisha Jibu hilo lilikasirisha bwana Msabila kufuatia kusubiri chakula hicho kwa muda mrefu na baada ya kujibizana ukatokea mzozo uliopelekea kutoelewana baina ya mama huyo aliyejulikama kwa jina moja la Amina ambapo walitukanana na baadaye bwana Msabila alirudi katika eneo lake la kazi na baada ya kukaa na kujisahau ambapo nbaada ya muda alishangaa kumuona Amina akija pale na sufuria ambalo lilikuwa na maji na baada ya muda mfupi mno kupita ,Amina alimmwagia maji ya moto na kuungua vibaya bwana Msabila na haraka haraka mama huyo alikwenda kiyuo cha polisi cha Mbezi kwa Yusuf na kufungua taarifa ya uongo kwamba amefanyiwa fujo na majeruhi huyo
Baada ya muda bwana Msabila alichukuliwa na wasamalia wema  na kupelekwa kituo cha polisi ambapo Askari aliyempokea kwa maelezo ya bwana Msabila alimwambia kuwa wewe ni mtuhumiwa umefanya fujo hivyo alimpatia PF3 ili aende kupata matibabu na baadaye aje afunguliwe mashtaka kufanya fujo.
Katibu Mkuu wa TAMRA Bwana Antony Sollo alipata taarifa na kuamua kwenda Hospitali ya Tumbi alipofika hospitalini hapo alishuhudia mwili wa bwana Msabila ulivyoungua vibaya  na maji ya moto ambapo alimpa pole na kuahidi kufuatilia suala hilo katika kituo cha polisi Mbezi kwa Yusufu
Akiwa njiani kuelekea mbezi alipigiwa simu na kujulishwa kuwa mtuhumiwa Amina tayari amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo alipofika kituoni hapo alimuona mtuhumiwa huyo na baada ya kumhoji hakuwa na la kusema na zaidi ya yote kujuta kwa kuchukua maamuzi mabaya kiasi hicho kwa kummwagia maji ya moto Bwana Msabila ambapo mtuhumiwa huyo amefunguliwa kesi ambapo namba ya kesi hiyo ni KMR/RB/157661/2012 kosa la kujeruhi.
Hali hii inathibitisha kuwa wapo kina mama wababe kuliko hata wanaume na hali hii ya kutokuwa na taarifa za ukiukwaji huu wa haki dhidi ya mwanaume ni kutokana na kutokuwa na chombo cha kuratibu matukio mbalimbali ambapo anapenda kuifahamisha jamii kuwepo kwa matukio ya ukiukwaji wa Haki yanayofanywa na wanawake .
 Katibu Mkuu wa TAMRA amelaani vikali ukatili uliofanywa na wanawake  na wanaume na kuwataka wananchi kuripoti matukio haya pindi yanapotokea ili kuwezesha kuwa na takwimu mbalimbali sahihi kuhusu ukatili unaofanywa na wanawake pia badala ya kuwa na takwimu za upande mmoja  wa wanaume,na ameitaka jamii ya Watanzania hususani wanaume kote Nchini kujitokeza katika kutoa taarifa za ukiukwaji wa Haki za Binadamu na ukatili kama huu bila woga maana hakuna mtu atakayewazomea kwani hii pia ni hali ya kwaida katika kupashana habari.

 Hapa ni Kibao cha Hospitali ya Tumbi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani


 Bwana Methody Msabila mwenye Pamba kifuani akiwa ametulia baada ya maongezi yake na Katibu Mkuu wa TAMRA hayupo pichani baada ya kutembelewa Hospitalini kujua hali yake.



Bwana Methody Msabila mwenye Pamba kifuani akiwa na wagonjwa wenzake katika Hospitali ya Tumbi

TAMRA itaendelea kuwapa taarifa mbalimbali kupitia blog yake ya www.tamratanzania.blogspot.com hivyo karibuni kila wakati muweze kuangalia matukio mbalimbali.
ASANTENI SANA NA POLENI KWA TAARIFA YA KUSIKITISHA.
UONGOZI WA TAMRA UNAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2013