Na Antony Sollo Mwanza
WANAFUNZI
wa Shule ya Msingi Buhongwa B iliyoko katika Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza
wanasoma wakiwa chini ya mti wakiwa hawana hata Madawati ya kukalia kufuatia
changamoto kubwa za Vyumba vya Madarasa Matundu ya vyoo na nyumba za walimu zinazoikabili
shule hiyo Tanzania Daima limebaini.
Mwandishi
wa Tanzania Daima aliyefika shuleni hapo alishuhudia wanafunzi zaidi ya mia
moja wakisomea nje chini ya miti huku kukiwa na wingu zito la mvua ambapo baada ya kufuatilia kwa wahusika kujua
tatizo ni nini walimu wa shule waligoma kueleza chochote na kumuomba Mwandishi
huyo akaonane na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba kwa kuwa yeye
ndiye msemaji mkuu.
Mwandishi
wa gazeti hili alimtafuta Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kuzungumzia suala hilo
ambapo alikiri kuwepo kwa upungufu mkubwa wa vyumba vya Madarasa.
“Tuna
changamoto kubwa ya vyumba vya Madarasa hii inatokana na idadi kubwa ya
wanafunzi ambapo kwa mwaka 2016 tuliandikisha wanafunzi 500 na mwaka 2017 hadi
jana 27 feb tumeandikisha wanafunzi 450 jumla ya wanafunzi wote kwa sasa ni 950
katika Shule hiyo”alisema Kibamba.
Akifafanua
Mikakati waliyo nayo Mkurugenzi huyo alisema kuwa Mwaka 2016 waliandikisha
wanafunzi 8000 katika Halmashauri ya
Wilaya ya Nyamagana na mwaka 2017 kuna wanafunzi zaidi ya 8000 ambapo mpango wa
Elimu bure ulitangazwa na Rais Magufuli umesababisha ongezeko kubwa la
wanafunzi na kuvuka malengokatika uandikishaji wa wanafunzi.
Hadi
Sasa Serikali imepeleka Shilingi mil 15,000,000 katika Shule hiyo kwa ajiri ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa huku Shilingi Mil 900,000,000 zikipelekwa Halmashauri
ya Wilaya ya Nyamagana ajiri ya kukamilisha mradi wa madawati ya akiba ili
kukabiliana na ongezeko lolote litakalojitokeza baada ya kukamilika kwa ujenzi
wa vyumba vya madarasa shuleni hapo
Kwa
upende wake Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula alikiri kuwepo kwa changamoto
zinazoikabili shule hiyo ambapo Mabula alisema kuwa ni kweli kuna upungufu
mkubwa wa vyumba vya Madarasa, Nyumba za walimu, matundu ya vyoo pamoja na
majengo ya Ofisi za Walimu.
“Tuna
uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa katika jimbo letu la Nyamagana lakini
pamoja na hayo tumejitahidi kwa upande wa Madawati tumefanikiwa kukamilisha
idadi inayotakiwa na hadi sasa tuna ziada ya madawati 3000 yakiwa hayana pa
kuyaweka.
Akizungumzia
mikakati waliyonayo kukabiliana na changamoto hizo Mbunge huyo alisema kuwa wanahamasisha
wadau mbalimbali ikiwemo Serikali kuu pamoja na wananchi katika maeneo
mbalimbali jimboni humo kuchangia ujenzi wa vyumba vya Madarasa vipatavyo 24
ili kuweza kuanzisha Shule mpya kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika shule
mbalimbali jimboni humo.
“Tuna upungufu wa vyumba vya Madarasa vipatavyo
1200 na hadi sasa tunaendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa
vyumba vya Madarasa vipatavyo 24 kwa ajiri ya kuanzisha Shule mpya ili
kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika shule mbalimbali katika jimbo
letu”.alisema Mabula.
MWISHO