TAMKO
LA CHAMA HA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA ( TAMRA )
25.02.2017.
Tamko la chama cha
kutetea haki za wanaume Tanzania kuhusiana
na tukio la mauaji ya yaliyofanywa
na Mohamed Mohamed mkazi wa boko Jijini Dar es salaam tukio ambalo
limeteka hisia za wengi kuwa mwanaume
huyo ametenda kosa bila kuangalia pande zote ili kujua chanzo cha tatizo la
wanandoa hao
Chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania TAMRA kimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya mauaji yaliyotokea huko boko Dar es salaam
kutokana na hatua zilizochukuliwa na mmoja wa wanaume aitwaye Mohamed Mohamed
(46) mfanyabiashara mkazi wa boko jijini
dar es salaam kwa kumuua mkewe sophia(36) na kisha yeye mwenyewe kujiua na
kuacha ujumbe kurasa 80 ujumbe ambao kwa
mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi ndiyo umebeba sababu mauaji hayo
Kimsingi,jamii imekwenda mbali katika tukio hili kwa
kuwachukulia wanaume kuwa ni wabaya,ni katili, sawa lakini chama hiki kinaomba
jamii itambue uwepo wa migogoro mikubwa inayofukuta ndani ya ndoa zetu huku
chanzo kikubwa kikiwa ni baadhi ya akina mama,nasema hivyo kutokana na ushahidi
kwamba,tafiti zilizofanyika hapo nyuma zilionyesha kuwa katika mikoa minne
ikiwemo lindi mtwara dar es salaam na zanzibar ilionyesha kuwa wanawake
walikuwa wakiongoza kwa kupiga wanaume ikiwamo kuwanyima unyumba huku wanaume
wakikosa pa kusemea kutokana na kutokuwepo kwa chombo hiki mpaka pale chama
hiki kilipoanzishwa .
Matatizo mengine ukiachilia kupigwa wanaume wamekuwa
wakipambana na vituko vingi ikiwemo ukatili wa kijinsia kwa kutengwa na familia
wakiwemo watoto kuambatana na misimamo ya mama huku baba akibaki mkiwa na
baadaye kupelekea vifo vingi kwa akina baba.
Tafiti zinaonyesha kuwa wanaoathirika zaidi ni wanaume hasa
waliostaafu kazi serikalini taasisi na mashirika kwamba wanapokuwa wamekoma
kupata fedha kwa ajiri ya kutunza familia hutengwa na baada ya muda huugua
magonjwa makubwa ikiwemo kupooza,sukari,nk.
Yote haya yanatokana na mwanaume kushindwa kuthaminiwa utu
wake na kudharauliwa na familia na hapo ndipo hujikuta katika lindi la mawazo
na kupelekea kupoteza maisha.
katibu mkuu wa chama cha kutetea haki za wanaume Antony Sollo
amejaribu kufuatilia suala hili kuona jamii imelipokeaje tukio hili ambapo watu
mbali mbali wameweza kuelezea hisia zao
akizungumza na katibu mkuu wa tamra seif hemed mkazi wa uhuru jijini mwanza ametoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo na kusema kwamba tukio hili limesababishwa na mwanamke kutokana na majibu aliyokuwa akimjibu mwanandoa mwenzake hususani pale alipotamka kwamba watoto waliozaa si wake,matumizi mabaya ya fedha za mmewe jambo ambalo linaumiza moyo
akizungumza na katibu mkuu wa tamra seif hemed mkazi wa uhuru jijini mwanza ametoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo na kusema kwamba tukio hili limesababishwa na mwanamke kutokana na majibu aliyokuwa akimjibu mwanandoa mwenzake hususani pale alipotamka kwamba watoto waliozaa si wake,matumizi mabaya ya fedha za mmewe jambo ambalo linaumiza moyo
“hata kama nngekuwa mimi nisingeweza kuvumilia kwa kuwa mke
nimeshiriki kumtafuita kumlipia mahari,kumtunza kwa kumpatia mahitaji
mbalimbali ikiwemo kulea ujauzito na kuwalea watoto nikijua ni mali yangu
halafu leo mtu anaibuka na kusema kuwa watoto hawa si wangu inauma sana alisema
seif”.
kufuatia hali hii tamra haina ugomvi na wanawake ila
inawataka wanandoa kuheshimu ndoa kwani ni agizo la mungu kwamba enendeni
mkazaliane muijaze dunia ambapo baada ya agizo hilo muungu aliagiza mambo
mawili ikiwemo wajibu wa kila mwanandoa.
iwapo wanandoa watamheshimu mungu na kutekeleza wajibu wao
kila mmoja ndoa hizo zitadumu na amani ndani ya ndoa hizo itakuwa ni ya milele.
Haya
ni
Maagizo ya mungu kwa wanandoa.
kwa
wanawake : WAEFESO 5 : 22 neno
la Mungu linasema enyi wake watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu , kwa
maana Mume ni kichwa cha Mkewe,kama kristo naye ni kichwa cha kanisa naye ni
mwokozi wa mwili lakini kama vile kanisa limtiivyo kristo vivyo hivyo wake nao
wawatii waume zao katika kila jambo.
Kwa
Wanaume: Waefeso 5: 25 Enyi waume wapendeni wake zenu kama kristo
naye alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajiri yake,ili makusudi alitakase na
kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu lisilo na ila
wala kunyanzi wala lolote kama hayobali liwe takatifu lisilo na mawaa vivyo hivyo
imewapasa waume zao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe ampendaye mkewe
hujipenda mwenyewe,hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote bali huulisha na
kuutunza kama kristo naye alivyolitendea kanisa.
Hivyo nachukua nafasi hii kuiomba jamii mambo yafuatayo
1.
Kuheshimu neno la Mungu ili kuweza kudumisha
ndoa zetu.
2.
Kuwa wavumilivu katika shida na raha kama viapo
tulivyoapa mbele za Mungu
3.
Tuweze kujifunza masomo ya ndoa ili kuingia
katika ndoa tukiwa na ujuzi juu ya wajibu wetu baada ya kuingia katika Tasnia
hii muhimu ya ndoa.
4.
Tumtegemee Mungu katika mambo yote na tukio
hili liwe fundisho kwetu tujipeleleze ni wapi tuna Mgogoro usioisha katika ndoa
zetu ili kuepuka Mauaji ya aina hii.
IMEANDALIWA
NA:
Antony
Johnson Sollo
KATIBU
MKUU TAMRA TANZANIA
1.
0767 203
556 BERENS CHINA Mwenyekiti TAMRA
2. 0762 117 117 ANTONY JOHNSON SOLLO Katibu
Mkuu TAMRA